Gari Moshi Laua Watu 20 Misri

KIMATAIFA
Rais wa Misri  Abdul Fattah al Sisi ametuma salamu za rambirambi kwa familia za marehemu waliopata  ajali ya treni katika njia kuu ya treni nchini humo na kusisitiza majeruhi wapate msaada wa haraka ili kuokoa misha yao. Takwimu za awali zinaeleza kuwa takribani Watu 20 wamekufa na wengine 40 kujeruhiwa kutokana na ajali hiyo iliyotokea baada ya treni hiyo kugonga kizuizi cha kupunguza kasi, katika kituo kimoja cha treni katikati ya mji na kusababisha kulipuka kwa tanki la mafuta la treni hiyo Watu walioshuhudia ajali hiyo wamesema wameona miili kadhaa katika janga baya kukumba nchi hiyo katika siku za hivi karibuni, hususan kwa usafiri wa treni. Mmoja wa mashuhuda, Ahmed Mahmoud ameliambia shirika la Habari la AFP, kuwa alitoa miili ya watu 20 na kuiweka kwenye gari la wagonjwa, yote ikiwa imechomeka. Aidha amesema kawaida treni likikaribia kituoni huja kwa mwendo wa taratibu, lakini siku hiyo lilikuwa katika kasi. Awali vyombo vya habari vya nchi hiyo viliripoti kwamba watu waliofariki ni 25 huku wengine 50 wakiwa wamejeruhiwa. Waziri mkuu wa nchi hiyo Mostafa Madbouli amesema atawachukulia hatua kali kwa yoyote atakaye bainika kuhusika kwa tukio hilo #BbcSwahili

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *