Taasisi ya Tulia Trust yafanikisha kugharamia matibabu ya Amos

KITAIFA

Taasisi ya Tulia Trust yafanikisha kugharamia matibabu ya kijana Amos Gabriel ya kwenda kutibiwa katika Hospitali Neurogen ya nchini India.

Kijana huyo na mzazi wake wanatarajia kuondoka Machi Tatu ikiwa taratibu zote za matibabu zimeshafanyika pamoja na gharama Hospitali hiyo zimeshalipwa tayari.

Akizungumza wakati kukabidhi Taasisi ya Tulia Trust na wadau mbalimbali wameweza kufanikisha sh. milioni 33 kwa matibabu ya kijana huyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi ya sh.milioni 33 kwa mzazi wa Amos amesema kuwa wanamuombea Mungu aweze kurejea katika hali yake ya kawaida na muendelea na masomo.

Amesema kuwa waliguswa baada ya kuona taarifa katika vyombo vya habari juu madhila yanayomkuta kijana huyo.Amesema kuwa kijana Amos ana ndoto ya shule hivyo isiweze kukatishwa.


Ameshukuru wadau kwa kuungana katika kufanikisha matibabu ya kijana huyo.Mzazi wa Amos amesema anamshukuru Naibu Spika kwa kijitoa na watanzania katika kufanikisha gharama ya matibabu ya kwenda kutibiwa nchini India.

Amesema kuwa kuwa yeye sio bora sana kwani kuna watu wengine wanataka msaada huo.Mgonjwa wa Amos Gabriel amesema kuwa anawashukuru watanzania kupitia Tulia Trust kwa kumuona inahitaji msaada baada ya kuona taarifa katika vyombo vya habari.

Gabriel anatatizo la uti wa mgongo uliotokana na kuanguka katika mti wakati akikata fimbo ya mwalimu kwa ajili ya kuwachapia wanafunzi.


 Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akipokea Mkono wa shukrani kutoka Amos ambaye anatarajia kwenda katika matibabu ya magogo nchini India. Balozi wa Tulia Trust Lameck Ditto akizungumza ana waandishi habari wa kuhusiana na Taasisi hiyo kutoa msaada kwa Amos kwa ajili matibabu nchini India.


Naibu Spika Dkt.Tulia Ackson akizungumza wakati alikwenda kupeleka msaada wa matibabu ya Amos nchini India ambayo Fedha hiyo imetolewa na Taasisi ya Tulia Trust na wadau wengine.Amos Gabriel akieleza namna ya umuhimu watanzania kuguswa na kuchangia kwa ajili ya matibabu ya nchini India.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *