Mtoto Wa Osama Aipasua Kichwa Marekani

KIMATAIFA

Marekani imetangaza dau la dola  milioni 1 kwa atakaye toa taarifa za upatikanaji wa mtoto  wa kiume wa kiongozi wa kundi la al-Qaeda – Osama Bin Laden, Hamza.

wizara ya mambo ya nje  nchini marekani inadai kuwa Hamza Bin Laden ni kiongozi mkuu wa kundi hilo la wapiganaji wa kiislamu,

Katika miaka ya hivi karibuni Hamza, ametoa kanda za video na sauti ambapo anatoa wito kwa wafuasi kuishambulia Marekani na washirika wake wa mataifa ya magharibi katika kulipiza kisasi kwa mauaji ya babake.

Hamza Bin Laden, anayeaminika kuwana umri wamiaka 30 alitangazwa rasmi na Marekani kama gaidi duniani miaka miwili iliyopita.

Amemuoa binti yake Mohammed Atta, aliyeiteka ndege mojawapo kati ya nne za abiia zilizotumika katika mashambulio hayo ya 2001, na kuivuruviza katika majengo ya World Trade Center mjini New York.

Vikosi maalum Marekani vilimuua babake Osama Bin Laden huko Pakistan mnamo 2011.

Aliidhinisha mashambulio dhidi ya Marekani mnamo Septemba 11 2001, ambapo takriban watu 3,000 waliuawa

#BbcSwahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *