Wakulima wa bangi watuhumiwa kuwasha moto Mlima Kenya

KIMATAIFA

Wakulima wanatuhumiwa kujihusisha na ulimaji wa zao la Bangi nchini Kenya wamesababisha moto katika eneo la misitu  ya  mianzi katika  Mlima  Kenya au Mount Kenya.

Tayari moto huo umeharibu kilomita 80 mraba za ardhi na sasa unatishia misitu ya jadi.

Kwa mujibu wa shirika la utafiti wa kimataifa wa ukulima CGIAR, ni sawa na takriban 3-4% ya misitu ya mianzi.na sasa unatishia mojawapo ya maeneo matano ya juu linalofahamika kama “water towers”, ambalo ni chanzo cha maji kwa mito na ndio chanzo cha robo tatu ya maji yanayosambazwa nchini.

Moto huo, ulianza siku saba zilizopita, unaawaka katika maeneo mawili na umekuwa ukisambaa kutokana na upepo na joto kali.

Shirika la Wanyama pori limeeleza kwamba limekuwa likiendelea na jitihada za kuudhibiti moto huo, na kwamba maafisa wa zima moto wamepiga kambi katika eneo hilo wakiendelea na jitihada za kuuzima moto.

Watu wa jamii kutoka eneo hilo wamekuwa wakisaidiana na maafisa wa misitu na mashirika ya kibinafasi ya kuhifadhi mazingira, ambao wana rasilmali msingi kukabiliana na ukubwa wa moto huo.

Wakulima wanatuhumiwa kuuwasha moto huo wanoajaribu kulisafisha eneo la ardhi ili kupanda bangi na sasa unatishia mojawapo ya maeneo matano ya juu linalofahamika kama “water towers”, ambalo ni chanzo cha maji kwa mito na ndio chanzo cha robo tatu ya maji yanayosambazwa nchini.

#BbcSwahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *