Acacia Kuwalipa Wananchi Fidia Ya Bill3.8

KITAIFA

Menejani wa idara ya Jamii Endelevu Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu ACACIA North Mara Uliopo Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara Richard Ojendo amesema mgodi huo unatarajia kuanza kulipa malipo yafidia ya ardhi kiasi ch Shilingi Billioni 3.8.

Akiongea na Waandishi wa habari Ojendo amesema zaidi ya Wananchi 200 kutoka vijiji Vilivyofanyiwa tathimini Mwaka 2011-2012 pamoja na awamu za 35, 41,na 42 katika vijiji vya Nyabichune, Mjini kati, Nyangoto, na Nyakunguru watalipwa fedha

Aidha amesema wananchi wa kijiji cha Nyabichune waliofanyiwa tathimini eneo la Makerero awamu ya 47 kwa waende kuechukua malipo yao ya fidia ifikapo 04 Machi Mwaka huu.

“Zoezi hili ni kwa wananchi halisi wa maeneo na awamua ambazo zimetajwa ambao taarifa zao zilichukuliwa na mgodi kwa ajili ya malipo ya fidia na orodha kamili wananchi watakaolipwa tayari tumekabidhi viuongozi wa vijiji na vitongoji huska” amesema  Ojendo.

Pia Ojendo  aliongeza kuwa malipo kwa awamu nyingine yataendelea kulipwa na wahuska watajulishwa pale muda utakapofika na kuomba wananchi kuendelea kutoa ushirkiano mkubwa dhidi yao na Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu ACACIA North Mara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *