Helikopta Yauwa Watano Kenya, Akiwemo Rubani Wa Makamu Wa Rais

KIMATAIFA

Takrikabi watu watano akiwemo Rubani wa Naibu Rais wa Kenya, Kapteni Mario Magonga, wamefaariki dunia baada ya helikopta aliyokuwemo kuanguka nchini Kenya.

Kwa mujibu wa vyombo vya usalama na Habari nchini Kenya helikopta hiyo ilianguka Jumapili muda wa saa mbili usiku katika eneo la Labolo, kisiwa chenye milima ya volcano katikakati ya ziwa Turkana – Central Island National Park kaskazini magharibi mwa Kenya.

Kapteni Mario Magonga ni Rubani wa Naibu Rais wa Kenya William Ruto.

Inaarifiwa kwamba vikosi vya usalama vimetumwa katika eneo hilo katika kusaidia kwenye jitihada za kuondosha miili na masalio ya ndege hiyo.

Kufikia sasa, chanzo cha ajali bado hakijajulikana

#BbcSwahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *