PICHA MAZISHI YA RUGE MUTAHABA

HABARI PICHA
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga, aakiweka mashada katika kaburi la marehemu Ruge Mutahaba ambaye amezikwa leo kijijini kwao Kiziru Bukoba,Shughuli za maziko zilianza kwa Ibada ya mazishi ambayo iliongonzwa na Katibu wa Parokia ya Itahwa, Anatory Kyatwa huku nyimbo za kihaya zikipamba tukio la mazishi.

Wazazi, familia, wakiweka shada la maua katika kaburi la mpendwa wao,marehemu Ruge Mutahaba ambaye amezikwa leo kijijini kwao Kiziru Bukoba.Katika shughuli hiyo viongozi mbalimbali wa Serikali wameshiriki,wakiwemo wasanii wa Bongo Muvi,Muziki,marafiki,ndugu na jamaa kutoka sehemu mbalimali walitoa heshima yao ya mwisho kwa mpendwa wao Ruge  katika Viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba kabla ya kuzikwa kijijini kwao.

Mkuu wa MKoa wa Dar Es Salmaa,Paul Makonda akiweka maua katika Kaburi la Ruge.


Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, January Makamba akiweka shada.
Awali wakati wa tukio la kuaga mwili wake katika viwanja vya Gymkhana, Maaskofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba walimtaja Ruge kama kijana jasiri mzalendo na mfano wa kuigwa.


Askofu Desderius Rwoma ameitaka jamii kuenzi mambo mema aliyoacha huku msaidizi wake, Methodius Kilaini akisema vijana wengi wamepata mafanikio kutokana na udhubutu wake na ujasiri wa kusimamia anayoamini.


M
ama wa marehemu Ruge Mutahaba (wa pili kushoto), akifuatiwa na mumewe wakiwa na aliyekuwa Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandala, dakika chache kabla ya mwili wa mtoto wao marehemu Ruge Mutahaba Kuingizwa kaburini, kijijini Kiziru. Rip Ruge

M

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *