RC Rukwa Awapongeza Viongozi Wilaya Ya Nkasi

KITAIFA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameupongeza Amepongeza ushirikiano unaoonyeshwa na uongozi wa wilaya ya Nkasi unaoongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo mh. Said Mtanda pamoja na wabunge, madiwani na mkurugenzi.


wangabo alitoapongezi hizo wakati wa ziara yake ya kutembelea ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi pamoja na ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga ili kujionea changamoto mbalimbali zinazoukabili mradi huo ambao unatakiwa kuisha mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka huu.


aidha amewataka wakuu wa Wilaya za Mkoani Rukwa kuhakikisha wanakuwa na utaratibu wa pamoja katika kutembeleana na kuelezana changamoto na mafanikio katika maeneo ya mradi wa ujenzi wa hospitali za wilaya ili kujenga hospitali hizo katika hadhi sawa na hatimae kupeana ujuzi wa utekelezaji wa mradi huo.


“Wakuu wa Wilaya waweke program ya kutembeleana kwa pamoja ili kujifunza, wanakuja kwa mfano (wilaya ya) Nkasi, wanakwenda wilaya ya Sumbawanga, Wanakwenda wilaya ya Kalambo halafu watakaa chini wafanye tafakari ili waone ni namna gani wanweza wakasimamia vizuri hizo hospitali zetu za wilaya kwasababu tunapaswa tuwe na kitu bora, hospitali zote tatu ziwe bora ndani ya mkoa wetu,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *