Mwalimu Alimuua Mwanafunzi Ahukumiwa Kunyongwa

KITAIFA

Mwalimu wa shule ya Msingi Kibeta iliyopo mkoani Bukoba, Respicius Patrick amekutwa na hatia na Mahakama Kuu Kanda mkoa huo na kuhukumiwa kukunyongwa hadi kufa.

Mwalimu Patrick alitiwa hatiani kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa darasa la tano, Sperius Eradius

Tukio hilo lilitokea baada ya mwanafunzi huyo kupigwa na mwalimu wake wa kiume, Respicius Patrick akimtuhumu kuiba mkoba wa mwalimu Herieth Gerald, ambapo ilikuja kubainika kuwa mkoba huo ulikuwa umesahaulika kwenye Pikipiki aliyokuwa amepanda.

Hata hivyo mahakama hiyo imemwachia huru mwalimu Herieth Gerald, baada ya kujilidhisha kuwa hana kosa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *