TAKUKURU Ruksa Kumohoji Malinzi

MICHEZO NA BURUDANI

Wakili wa Serikali wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Leornad Swai kumhoji aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi na Katibu wake, Selestine Mwesigwa.

Shauri hilo liliwasilishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, baada ya shahidi wa 11 katika kesi hiyo kumaliza kutoa ushahidi wake.

Swai amedai kuwa Januari 16, 2019 waliomba kuwahoji washtakiwa hao, lakini hawakuweza kwa sababu walitoa sababu zao kuwa wahojiwe siku nyingine. Hakimu Kasonde alikubaliana na ombi hilo na kutoa ruhusa kwa TAKUKURU kuwachukua kwa ajili ya mahojiano

Hakimu Kasonde alisema washtakiwa hao watahojiwa Machi 8, 2019 na kesi itaendelea kusikilizwa Machi 19,2019.

Malinzi na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 28 yakiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni USD, 375,418.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *