MBUNGE MAVUNDE AWATAKA WANAWAKE DODOMA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI

KITAIFA

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amewataka wanawake wa Dodoma Mjini kuchangamkia fursa za kiuchumi na kutokubali kukatishwa tamaa kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi ili kujijengea heshima kubwa katika jamii.

Mavunde ameyasema hayo leo asubuhi katika kongamano lilioandaliwa na Chama cha Walimu Tanzania(CWT) kitengo cha Wanawake katika Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha siku ya MWANAMKE DUNIANI.

“Natamani kuwaona wanawake wa Dodoma mkiwa mbele kuchangamkia fursa za kiuchumi ili kujijengea nguvu ya kiuchumi na kujiongezea kipato.Dodoma hivi sasa baada ya tamko la Makao Makuu fursa nyingi sana zimejitokeza hivyo msilaze damu kwa kubaki kuwa waangaliaji na badala yake na ninyi mshiriki moja kwa moja”Alisema Mavunde

Akisoma Risala kwa niaba ya walimu hao kitengo “KE” Mwl Joyce Kaishozi ameeleza kwamba Chama hicho kimejipanga vyema kumjengea uwezo mwalimu mwanamke ili jamii kutambua nafasi ya Mwalimu Mwanamke na ndio maana katika kongamano walimu wamepata nafasi kupata mafunzo katika maeneo ya AFYA,*UJASIRIAMALI na UONGOZI BORA.

Kongamano hilo pia lilihudhuriwa na Mjumbe Wa Kamati Kuu CCM na Mlezi wa Mkoa wa Dodoma Ndg Leila Burhan Ngozi na Mbunge wa Viti Maalum-Dodoma Mh Felister Bura

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *