Meneja Wa Donald Trump Ahukumiwa Kifungo Jela

KIMATAIFA

Aliyekuwa Meneja kampeni za rais wa Marekani Donald Trump Paul Manafort amehukumiwa kifungo cha miezi 47 jela kwa udanganyifu katika ulipaji wa kodi na benki.

Manafort Alipatikana na hatia mwaka jana kwa kuficha mamilioni ya dola wakati alipokuwa balozi nchini Ukraine.

Hata hivyo Anatarajiwa kuhukumiwa katika kesi nyingine wiki ijayo kwa kufanya kampeni kinyume cha sheria.

Mashitaka hayo yalitokana na na uchunguzi uliofanyika juu ya ikiwa maafisa wa kampeni ya Trump walifanya njama na Urusi ili kumuwezesha apate ushindi katika uchaguzi wa 2016.

Balozi maalumu wa wizara ya sheria ya Marekani Robert Mueller anatarajiwa kukamilisha uchunguzi wake wa miezi 22 ambao unalenga urais wa Trump

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *