OSHA Yatoa mafunzo kwa Wanawake wanaofanya usafi Barabarani

KITAIFA

Wakala wa Usalama na Afya Pahala Pa Kazi (OSHA)imesema kuwa nguvu kazi ya Taifa lazima ilindwe katika afya ili iweze kuzalisha kwa kujenga uchumi wa nchi.

Hayo ameyasema Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda wakati wa mafunzo ya wafanyakazi wanawake wanaofanya usafi katika barabara za Manispaa ya Kinondoni na Ilala amesema kuwa wanawake ndio wazalishaji pamoja na wasimamizi wa familia hivyo serikali inaangalia katika jicho ya kulinda afya zao wasiweze kuteteleka na kushindwa kusimamia familia zao.

Amesema kuwa wanawake hao wanaweza kuwa wanafanya usafi lakini hawafahamu jinsi ya kulinda afya zao ambapo OSHA ndio kazi yao katika kuwajengea uwezo wa kutambua umuhimu wa afya zao katika sehemu za kazi zao.

Mwenda amesema kuwa katika kuelekea siku ya kilele cha maadhimisho ya siku wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 ya kila mwaka OSHA imeona ni wakati mwafaka kutoa elimu ya wafanyakazi wanawake wa usafi katika baadhi ya barabara katika jiji la Dar es Salaam.

Aidha Mwenda amesema kuwa OSHA itaendelea kutoa elimu katika mahala pa kazi katika kuhakikisha uchumi wa viwanda unajengwa na nguvu kazi yanye afya imara.” Tumedhamiria kutoa elimu pahala pa kazi katika kuimarisha Afya za wafanyakazi ya kutokuwa na madhara ya kazi kwa kuwa wana vifaa vya kuzuia madhara hayo”amesema Mwenda 

Amesema kauli mbiu ya OSHA katika siku ya wanawake ni ‘Usalama wa Afya kwa kuzinagatia Usawa wa Kijinsia, Badiri Fikra Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu.Katika mafunzo hayo OSHA imetoa vifaa kinga kwa wanawake hao ili waweza kutekeleza majukumu yao katika kujilinda na afya na usalama sehemu zao za kazi.

Nae Mfanyakazi wa Usafi Barabarani Halima Rajab amesema wanachangamoto kwa madereva ambao huwa wanawafaya kuwa waangalifu na bila kufanya hivyo wanagongwa.

Amesema wanaishukuru OSHA kwa kuwaandalia mafunzo kwani wanaamini serikali imewaona. Maendeleo ya Uchi kuhakikisha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *