Polisi wazuia maadhimisho ya wanawake Chadema

KITAIFA

Jeshi la Polisi wilayani Geita limekizuia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

Katiba barua iliyotolewa na mkuu wa polisi wilaya, Ally Kitumbu iliyotolewa jana Alhamisi Machi 7, 2019 kwa katibu wa Chadema Geita yenye kumbukumbu namba GE/B.3/24/VOL.V11/63 imewataka wanawake kushiriki maadhimisho hayo maeneo ya Bugulula halmashauri ya wilaya na viwanja vya soko jipya yanakoadhimishwa na halmashauri ya mji.

Chadema walipanga kufanya maadhimisho hayo katika ukumbi wa Moyo wa Huruma uliopo mjini Geita na kutaka wanawake wa chama hicho kuungana na wanawake wenzao katika maadhimisho ya kiserikali.

Kila Machi 8 ya kila mwaka, wanawake duniani huadhimisha siku ya wanawake duniani

#Mwananchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *