Tfda Kanda Ya Kati Yaanza Kutoa Elimu Kuhusu Madhara Ya Vipodozi Kwa Wanafunzi Wa Shule Za Sekondari

KITAIFA

MAMLAKA ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Kati Dodoma imeanza kutoa mafunzo ya namna ya kudhibiti natumizi ya vyakula,dawa,vipodozi pamoja na vitendanishi kwa lengo la kutoa elimu kwa shule 30 za sekondari zenye jumla ya wanafunzi 12,000.

Mkaguzi wa TFDA Kanda ya Kati,Abeli Daule aliyasema hayo alipokuwa akitoa elimu juu ya bidhaa ambazo Mamlaka ya Chakula naa Dawa inadhibiti zikiwemo bidhaa za chakula,dawa,vifaa tiba na vitenganishi katika shule nane za sekondari za Halmashauri ya wilaya ya Singida.

Aidha Daule ambaye pia ni Afisa elimu kwa umma wa TFDA aliweka bayana lengo la kutoe elimu katika shule za sekondari kuwa ni sehemu za kazi ya Mamlaka hiyo kutoa elimu na kwamba sekondari ni wanafunzi wengi ambao tayari wanajitambua, kukiwepo watumiaji.

“Lakini pia sekondari wanafunzi ambao wengi tayari wanajitambua kwa maana kwamba wengine ni watumiaji lakini na wengine majumbani kwao wanatumwa,lakini pia ni muda ambao wakipewa elimu wanaweza kujua kufanya uchaguzi sahihi lakini pia watapeleka elimu hiyo nyumbani.”alisisitiza Mkaguzoi huyo.

Kwa mujibu wa Daule endapo wanafunzi hao wa sekondari watapatiwa elimu itasaidia pia kwa namna moja au nyingine kuwadhibiti wafanyabiashara wasio waaminifu wenye utamaduni wa kuikwepa serikali wanapobaini Mamlaka hiyo inafanyakazi, huamua kufunga biashara zao kutoweka kabisa.

“Kwa hiyo utaratibu huo ni wa taasisi kwa maana kwamba Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati katika utekelezaji wa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2018/2019 basi tumeona tupite katika hizi shule ili tuweze kuwapitia.”alibainisha Daule.

Naye Kaimu Afisa elimu sekondari wilaya ya Singida,Wolta Jenaeli aliweka bayana manufaa ya mpango huo utasaidia kwa akiasi kikubwa sana kwenye shule 30 zilizopo katika Halmashauri hiyo kupunguza madhara yatokanayo na vipodozi hususani kwa wanafunzi wa kike ni makubwa sana.

“Kwa hiyo ina maana tunapunguza zinazotokea kwenye mashule yetu kwa sababu umri wa watoto wetu walionao kutumia kila kitu bila kujua madhara yake ni yapi.”alisema kaimu afisa elimu wilaya ambaye pia ni afisa elimu sekondari wa wilaya hiyo.

Alizitaja baadhi ya shule za sekondari zilizopatiwa elimu hiyo kutoka TFDA kuwa ni pamoja na Ntonge,Amana,Mrama,Kijota, Kijota Hull,Mtinko,Singitu na Mikiwu.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi walionufaika mpango huo kutoka shule ya sekondari Kijota,Hajra Juma alisema mpango huo utawasaidia baadhi ya wanafunzi walioanza kutumia vipodozi hivyo endapo wataendelea kutumia vipodozi hivyo.


 Mmoja wa Maafisa wa TFDA Kanda ya Kati akielezea madhara ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kutumika kutokana na muda wake wa matumizi kwisha alipokuwa akitoa elimu ya madhara hayo kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Ntonge,wilaya ya Singida Vijijini.   Mkaguzi wa TFDA Kanda ya Kati,Abeli Dauli akitoa elimu katika shule ya sekondari Singitu,Halmashauri ya wilaya ya Singida juu ya madhara ya matumizi ya vipodozi vilivyokwisha muda wake.Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kijota wakiwa katika viwanja vya shule hiyo wakiwasikiliza  maafisa wa TFDA kutoka Kanda ya Kati walipokuwa wakitoa elimu juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya vipodozi vyenye viambato vyenye sumu.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *