Watu 152 Wafariki Kwa Ajali Ya Ndege Ethiopia

KIMATAIFA

Takriban wasafiri 149 kutoka nchi 33 na wahudumu wanane waliokuwa wakisafiri kwa ndege ya Ethiopian Airlines aina ya Boeing 737  kutoka Adis Ababa, Ethiopia kuelekea Nairobi, Kenya wamefariki kwa ajali ya ndege.

Kwa mujibu wa Taarifa toka Shirika la ndege la Ethiopia- (Ethiopian Airlines) ndege hiyo ilipata ajali baada ya kupoteza mawasiliano dakika sita baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Adi Ababa.

Taarifa ya Kampuni ya ndege ya Ethiopian Airlines imesema abiria kutoka nchi 33 waliosafiri kwenye ndege iliyopata ajali wote wamekufa, kulingana na Msemaji wa Kampuni hiyo Asrat Begashaw.

Taarifa ya Shirika la ndege la Ethiopia- Ethiopian Airlines inasema walipoteza mawasiliano na ndege iliyopata ajali dakika sita baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Adi Ababa.

Mkurugenzi mtendaji wa Ethiopian Airlines CEO Tewolde Gebremariam ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba miongoni mwa waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni pamoja na

Wakenya32 Kenyans, raia wa Canada 18 raia tisa wa Ethiopia , wataliano wanane , Wachina wanane, wamarekani wanane , waingereza saba , Wafaransa saba , Wamisri sita, Wajerumani watano , Wahindi wanne na wanne kutoka Slovakia.

Waastralia watatu, Waswis watatu, Warusi watatu , three Russians, Wakomoro wawili, Wahispania wawili, Wapoland wawili, Waisraeli wawili.

Kulikuwa pia abiria mmoja mmoja kutoka nchi za ubelgiji, Indonesia, Somalia, Norway, Serbia, togo, Msumbiji, rwandsa, Sudan, Uganda na Yemen.

Ndege hiyo ilitarajiwa kuwasili mjini Naorobi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo kanyatta saa nne unusu kwa saa za Afrika Mashariki.


Ndege ya Ethiopian Airlines Boeing 737 iliyoanguka

Shughuli za uokozi zikiendelea kwenye eneola tukio la ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines Boeing 737

Mkurugenzi Mkuu wa Ethiopian Airlines akiwa katika eneo la tukio la ajali

#BbcSwahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *