Watu 49 Wauwawa Wakifanya Ibada Msikitini

KIMATAIFA

Watu wenye silaha wanaodhaniwa kuwa ni magaidi wamewauwa watu 49 na wengine zaidi ya kumi wamejeruhiwa nchini New Zealand.

Tukio hilo limetokea katika jiji la Christchurch nchni humo kwenye misikiti miwili tofauti wakati watu hao wakifanya ibada ya ijumaa.

Katika taarifa iliyorushwa na kituo cha CNN, Waziri Mkuu wan chi hiyo Jacinda Ardern, amesema kuwa washambuliaji hao walikuwa na mtazamo wa imani kali ya kidini ambazo sio msingi wa utamaduni wa New Zealand pamoja na dunia kwa ujumla.

Naye Mkuu wa polisi wa nchi hiyo, Mike Bush amesema kuwa watu wanne wanashikiliwa kutokana na tukio hilo, ambao ni wanaume watatu na mwanamke mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *