Wizara Ya Afya Yatoa Elimu Ya Meno Kwa Watoto

KITAIFA

Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya kinywa na meno duniani, Wizara ya Afya Zanzibar kupitia Kitengo cha kinywa na Meno Hospitali Kuu ya Mnazimmoja kimetoa elimu ya utunzaji na uchunguzi wa meno na kinywa kwa watoto wanaolelewa katika nyumba ya watoto Mazizini.

Mkuu wa Kitengo cha Meno na Kinywa Hospitali kuu ya Mnazimmoja Dk. Semeni Shaban Mohd  alisema zoezi la kuwafanyia uchunguzi watoto lilianza mwanzoni mwa wiki hii katika shule mbali mbali za mjini na mashamba Unguja na Pemba.

Amesema zoezi hilo litaendelea hadi tarehe 20 mwezi huu siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya kinywa na meno duniani ambapo kwa Zanzibar itaadhimishwa katika Uwanja wa Mapinduzi Square Michenzani.

Aidha amewashauri wananchi kujitokeza katika maadhimisho hayo ambayo yataambatana na uchunguzi wa kinywa na meno kwa watu wote watakaofika siku hiyo na watakaobanika kuwa na matatizo watapatiwa matibabu bila malipo.

Kaulimbiu ya siku ya kinywa na meno duniani mwaka huu ‘Tufanye mdomo uwe na afya bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *