Ngome ya CUF Shinyanga Yabomoka, Wanachama Watimukia ACT – Wazalendo

KIMATAIFA
Spread the love

Takribani zaidi ya wanachama 200 wa Chama cha wananchi CUF wilaya ya Shinyanga mjini, wakiwemo viongozi wa cha hicho wamehamia ACT- Wazalendo kwa madai ya kutokubaliana na madai ya mahakama ya kumpa Profesa Ibrahimu Lipumba uenyekiti wa chama hicho.

Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wananchi CUF wilaya ya Shinyanga Mjini Said Juma Issa wakati wakihama chama hicho kwenda ACT-Wazalendo, alisema wameamua kuondoka kwenye chama hicho kwa hiari yao wenyewe bila ya kushawishiwa na mtu.

Naye Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo wilaya ya Shinyanga Mjini Twaha Makani, aliwapokea wanachama hao wapya kutoka chama cha wananchi CUF, huku akiwataka wafuate misingi na katiba ya chama hicho, ili kukijenga chama ambacho kwa sasa ndiyo kinaaminiwa na watanzania kuwaletea ukombozi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *