Maajabu Nyuki Waishi Ndani Ya Jicho La Binadamu

KIMATAIFA
Spread the love

Mwanamke mmoja nchini Taiwan mwenye umri wa miaka 28 , aliyejulikana kama bi He amepatikana na nyuki wanne wa sukari waliokuwa wakiishi ndani ya jicho lake,

Kisa hicho cha kwanza katika kisiwa hicho kilitokea wakati Bi He akipalilia makuburi ya watu wa jamii yake ndipo  nyuki hao waliporuka na kuingia katika jicho lake la kushoto.

Daktari Hong Chi Ting wa chuo kikuu cha hospitali ya Fooyin aliambia BBC kwamba alishangazwa wakati alipowatoa wadudu hao kwenye macho.

Bi He ametolewa hospitalini na anatarajiwa kupona kabisa. Nyuki wanaofuata jasho huvutiwa na jasho na mara nyengine huwarukia watu ili kung’ong’a jasho.

#BbcSwahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *