Chombo cha anga cha Israel chaanguka mwezini

KIMATAIFA
Spread the love

Chombo cha wana anga wa Israel kwa jina Baresheet kilichokua kikisafiri kuelekea mwezini kimeanguka baada ya injini yake kushindwa kufanya kazi.

Chombo hicho kilijaribu kutua kwenye mwezi lakini kikapata tatizo la kiufundi, Sababu ya safari hiyo ya mwezini ilikua kupiga picha na kufanya majaribio.

Mashirika ya anga ya Jumuia ya zamani ya kisovieti,Marekani na China pekee ndio walifanikiwa kutua salama kwenye mwezi.

Israeli ilikua na matumaini ya kuwa nchi ya nne kufanya hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *