Mume Amchoma Visu Mkewe

KIMATAIFA
Spread the love

Mwanamke mwenye umri wa miaka 30, mkaazi wa Karatina nchini Kenya, amenusurika kifo baada kuchomwa kisu mara 17 na mumewe kufuatia ugomvi wa kifamilia.

Peninah Wangechi, ambaye ni mama wa watoto watatu alikutwa na janga hilo Jumanne usiku wiki hii, alipokuwa akigombana na mumewe, Samuel Ndirangu.

Ndirangu alimchoma visu mkewe katika maeneo ya mgogo, usoni na kifuani na kisha kukimbia.

Akizungumza akiwa katika kitanda cha hospitali ya Karatina, Wangechi amesema kuwa ndoa yao imekuwa ngumu na yenye ugomvi mkubwa mara kwa mara ambao huhusisha kushambuliana.

Mganga wa zamu wa hospitali hiyo, Dkt. Benson Ngari ameiambia Citizen kuwa hali ya mwanamke huyo inaendelea kuimarika na kwamba kwa bahati nzuri majeraha ya visu hayakuchimba sana mwili.

Jeshi la polisi la eneo la Karatina limeeleza kuwa Ndirangu alijisalimisha baadaye katika kituo cha polisi na anashikiliwa kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *