Jukumu langu lilikuwa kutekeleza ahadi ya Mwalimu Nyerere – Rais Magufuli

KITAIFA
Spread the love

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa ni lazima kutekeleza masuala mbalimbali  aliyoyaahidi Watanzania wakati akiingia madarakani mwaka 2015, ambayo yanalenga kuwaletea wananchi maendeleo.

wakati alipokuwa akizindua mji wa Serikali uliopo katika kata ya Mtumba jijini Dodoma, Rais Magufuli alisema kuwa  aliamua kutimiza ahadi ya Rais wa Awamu ya Kwanza, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyoitoa mwaka 1973 ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi.

 “Nataka yote tuliyoyaahidi tuyatekeleze, nataka ofisi hizi nzuri tulizojenga ziwe na watu, na zianze kutoa huduma kwa wananchi” amesema.

 “Jukumu langu lilikuwa kutekeleza ahadi ya Mwalimu Nyerere, na  nilipata nguvu baada ya kukumbuka kuwa ziko nchi nyingi tu duniani ikiwemo nchi za Afrika kama Nigeria na Cote d’Ivoire ambazo zilihamisha makao makuu  ya nchi yao katika kipindi kifupi, nataka kuwahakikishia na mimi nakuja Dodoma  kwa sababu hakuna kinachonichelewesha,” amesisitiza.

Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa Serikali inaendelea kukamilisha  mifumo na ujenzi wa miradi mbalimbali kwa ajili ya kutoa huduma kwa watumishi wa umma ambao watahamia na kufanya kazi katika majengo hayo ikiwa ni pamoja na kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wanaofika katika mji huo wa Serikali, ikiwa ni  sambamba na kuboresha jiji la Dodoma.

Alitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa barabara itakayogharimu bilioni 500 kwa mkopo wa fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itakayojengwa kutokea  Mtumba, Veyula na Nala ambayo ina urefu wa kilomita 4.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *