Mbunge wa Viti Maalumu CCM akabidhi vitabu 120

KITAIFA
Spread the love

Na Amiri kilagalila-Njombe

Mbunge wa Viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe Dkt.Susan Kolimba amekabidhi Vitabu vya sayansi 120 vya Silabasi kwaajili ya wanafunzi wa kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari Mundindi iliyopo wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe.

Licha ya kukabidhi Vitabu hivyo, Dkt.Susan Kolimba pia amekabidhi vifaa vya michezo ambavyo ni Jezi seti mbili moja kwaajili ya Wavulana na moja kwaajili ya Wasichana pamoja na mpira mmoja, vilivyo gharimu pesa za Kitanzania zaidi ya Milioni tatu.

Kolimba amekabidhi vifaa hivyo alipo kuwa mgeni Rasmi katika Mahafali ya kwanza ya Kidato cha sita, iliyo fanyika April 12/2019 shuleni hapo huku akiahidi kushirikiana na uongozi wa shule hiyo kutatua baadhi ya changamoto zinazo ikabili shule ikiwemo kutafuta Kompyuta kwaajili ya matumizi ya walimu.

Aidha Mbunge huyo ameahidi kushirikiana na uongozi wa shule pamoja na kata ya Mundindi kuhakikisha anashiriki kusuka mfumo wa umeme katika Madarasa matano ya kuanzia shuleni hapo ili ibaki kazi ya kuingiza umeme kupitia REA kwakuwa nguzo za umeme huo tayari zimesha fika shuleni hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *